Loading...
 

Klabu za Rejea

 

Klabu ya Rejea ni tuzo ya heshima ambayo inatolewa kwa Klabu ya Umma yoyote ambayo inafanya vizuri kwenye vipengele vyote vya Mundo wa Kieliemu wa Agora na unazingatia miongozo yote ya kielimu na uendeshaji. Ni klabu ambayo klabu zingine zinaweza zikaitumia kama rejea au muundo wa kuufuata, mfano wa klabu inayoendeshwa vizuri.

Agora Speakers International itatangaza wazi wazi Klabu za Rejea ili kuwavutia watu, mashirika na vyombo vya habari.

Vigezo

Ili kuzawadiwa tuzo ya klabu ya rejea, klabu ya umma inatakiwa kufuata vigezo vifuatavyo:

Mahitaji ya Uanachama na kishirika

  • Lazima iwe na uwepo wa japo miezi 6 mfululizo
  • Ina uanachama imara, sio ambao unayumba yumba sana
  • Ina seti kamili ya Maofisa wa Klabu
  • Haina nyongeza ya maofisa ambao ni maalum kwa ajili ya klabu tu.
  • Haina vizuizi vya maudhui ya hotuba (zaidi ya vizuizi vya kawaida, vya Agora yote)

Uzingatiaji wa Kielimu

  • Klabu ina Mkakati wa mwaka mzima na seti ya malengo yaliyotengenezwa na Rais.
  • Klabu ina Mpango wa Kielimu wa mwaka mzima uliotengenezwa na Makamu wa Rais wa Elimu.
  • Klabu inafuata mapendekezo ya kwenye Mwongozo wa Uendeshaji kuhusiana na idadi ya shughuli/matukio kwa mwaka wa elimu.
  • Majukumu yote ya mkutano yanafanywa na yanatathminiwa kulingana na mwongozo wa majukumu.

Mahitaji ya Mkutano

  • Wanakutana uso kwa uso japo mara mbili kwa wiki (mara mbili kwa mwezi, kila mwezi isipokuwa kwenye miezi ya likizo ya nchi)
  • Ina mahudhurio ya japo wanachama 12 kwa mkutano, kwa wastani wa miezi 6 iliopita. Wanachama wanaohudhuria sio lazima wawe hao hao kila mara. Lakini kumbuka, kuwa wageni na wanaotembelea klabu hawahesabiwi kwenye idadi hiyo.
  • Kama mkutano una hotuba moja tu, lazima iwe mradi kutoka Njia ya Kielimu ya Agora. Kama mkutano una hotuba zaidi ya moja, japo mmoja unaweza ukawa kutoka mpango usio wa Agora.
  • Wageni wanakaribishwa vizuri na wanapewa kifurushi cha kuwakaribisha.

Mawasiliano

 

 

Kupata cheo cha rejea

Wadhifa wa klabu ya rejea unatolewa kama ifuatavyo:

  • Rais au Makamu wa Rais wa Elimu anatuma aidha muhtasari kupitia mfumo wa usimamizi wa mtandaoni wa klabu au kwa kutuma ujumbe kwenda info at agoraspeakers.org.
  • Ombi linatathminiwa, na ustahiki wa klabu unaangaliwa kutokana na rekodi zake. 
  • Tunaweza tukahudhuria mkutano mmoja au miwili ili kuhakiki jinsi masuala ya klabu yanavyoshughulikiwa. 
  • Kama kila kitu kipo sahihi, Cheo cha Rejea kitatolewa rasmi. Kama kuna suala lolote, tutatoa mwongozo wa jinsi ya kuyashughulikia, na klabu inaweza ikaomba tena pale yatakapotatuliwa.
Cheo cha Rejea ina uhalali wa mwaka mmoja, baada ya hapo lazima utafutwe upya.

Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:46 CEST by agora.